SAUTI YA VITA
UBATIZO WA MAJI -
(OUTLINE ON WATER BAPTISM)
Aggressive Christianity Missions Training Corps [ ACMTC]
International Generals James & Deborah Green
Jina Katika Ubatizo
Wakati mwamini anapobatizwa katika jina la Bwana Yesu, anamvaa Kristo, kama Paulo
anavyotuambia katika Wagalatia 3:27. “Ubatizo kwa maana hii ni sawa na ndoa.
Wakati mwanamke anapoolewa anachukua jina la mume wake, na kuingia kwenye
milki ya mume na anazo haki kamili nyumbani kwa mume wake.”
Hivyo ndivyo inavyokuwa mwamini anapobatizwa katika Jina la Bwana Yesu anavaa
jina la Bwana Yesu.
Sio tu kwamba anavaa lile jina, bali anachukua haki zote za halali na upendeleo wote
katika Kristo.
Wakati tunapobatizwa katika jina la Baba, inatupa nafasi ya mwana na upendeleo wa
mwana, urithi na utajiri wa mtoto.
Tunabatizwa katika ulinzi na utunzaji na ushirika wa Mungu hapa duniani kama Baba.
Tunavaa yote ambayo muungano unamaanisha. Tuna msimamo na mwana, upendeleo
na mwana, wajibu wa mwana.
Tunakuwa kwa njia ya ubatizo huo warithi pamoja na Kristo na warithi wa Mungu.
Tunaingia katika utajiri wa urithi kutoka kwa Mungu wa ulimwengu na mbingu.
Wakati tunabatizwa katika jina la Roho Mtakatifu tunabatizwa katika jina, utajiri, nguvu,
hekima na utukufu wa Mungu unaowakilishwa duniani. Yote Roho aliyonayo
tunabatizwa kwayo.
Tunakuwa washirika wa Neema yake, wa hekima yake, wa uwezo wake, wa nguvu
zake, wa maisha yake.
Kwa hiyo tunapobatizwa kwa jina la Bwana Yesu yote ambayo jina linasimama kwayo
mbinguni ni yetu, kila ushindi mkubwa ambao Yesu alishinda katika kifo chake, na
kufufuka kwake ni yetu.
Je, ina maana gani kubatizwa katika jina? Chukua andiko hili, “Mkiwabatiza kwa Jina la
Baba na la Mwana na Roho Mtakatifu.”
Kiroho ina maana kwamba, tunabatizwa katika yote ambayo jina linamaanisha katika
mpango wa Ukombozi. Tunabatizwa katika kazi iliyokwisha ya Kristo katika ukamilifu
wake, na tunapokea utimilifu na ukamilifu.
Kila neema iliyodhihirika katika Kristo tunafunikizwa, tunazungushiwa, tupo katika hiyo.
Utimilifu wote na uzuri katika tabia na maisha ya Yesu ni yetu.
Paulo anasema “Mmekamilishwa katika Yeye.”
Ina maana katika fahamu za Paulo kwamba ukamilifu, utimilifu, katika ukamilifu wa
Kristo unahesabiwa katika sisi.
Paulo alisema “Maana ninyi nyote mliobatizwa katika Kristo mmemvaa Kristo.”
Fikiri juu ya wajibu ulioambatanishwa katika hilo. Fikiria juu ya utukufu uliofunikizwa
huko, fikiria juu ya baraka ambazo zimeambatana na kuongezeka kutoka huko.
Kubatizwa katika jina la Yesu Kristo, na kumvaa Kristo kuwa na jina la Kristo- ni
heshima kubwa kupita zote ambayo mbingu inaweza kutoa juu ya mwanadamu.
Ni kazi gani kubwa, zinaweza kufanyika kwa njia ya mwana mtakatifu Yesu! Bwana
anatuinua juu - Bwana anatuwezesha - kwa neema yake kuingia kwenye urithi wetu na
kutekeleza wajibu wetu katika familia yake ya ajabu.
Hakushinda ushindi wowote katika kazi yake ambao haukuwa kwa ajili ya kanisa.
Moyo unaweza kuwa mgumu kupokea, kwamba wakati tunabatizwa katika ukamilifu,
kumaliza kabisa utimilifu wa Yesu Kristo, ambaye katika ukamilifu wake sisi sote
tumepokea neema juu ya neema.
Urithi Wetu
Yote ambayo jina linasimama kwayo, mwamini anasimama kwayo mbele za Baba.
Unabatizwa katika haki halali kutumia jina. Unabatizwa katika wajibu wote wa Mwana
uliofunikwa na nguvu isiyo ya kawaida katika jina lile kuu.
Mungu atusaidie kwa njia ya nguvu yake Roho Mtakatifu kuingia katika utajiri wa urithi
katika Yeye.
Wakati aliposema “Nimepewa mamlaka yote mbinguni na duniani (Mathayo 28:18) Basi
enendeni mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi mst. 18- Basi yale mamlaka
aliyokuwa nayo ni yetu nasi tunasimama kama badala yake.
Waefeso 1:22. Paulo anasema “ akavitia vitu vyote chini ya miguu yake, akamweka
awe kichwa juu ya vitu vyote kwa ajili ya kanisa; ambalo ndilo mwili wake, ukamilifu
wake anayekamilika kwa vyote katika vyote.”
Haki yake ni yetu, Upendo wake ni wetu, Neema zote alizonazo maisha yake mazuri ni
yetu.
Wakati tunapomvaa Kristo katika ubatizo, kwa neema yake tunaweza kufurahia neema
zote.
Kama waamini, utajiri wote, neema zote ni zetu. Kwa imani tunampokea Kristo kama
mwokozi wetu na Bwana na tunapofanya hivyo, kila utajiri na urithi katika Kristo Yesu
unakuwa wetu mara moja.
Maana Tatu
Warumi 6:4 “Basi tulizikwa pamoja naye kwa njia ya ubatizo katika mauti yake, kusudi
kama Kristo alivyofufuka katika wafu kwa njia ya utukufu wa Baba vivyo hivyo na sisi
tuenende katika upya wa uzima.”
Ubatizo una umuhimu wa aina tatu.
1. Ni kifo na kuzika yaliyopita
2. Ni kufufuka katika upya wa uzima na uhusiano
3. Ni muungano na yule ambaye kwa jina lake umebatizwa
Tunapo batizwa katika jina la Baba.
Hii ina maana umwana pamoja na upendeleo wote ambao unakuja na uhusiano wa mtu
wa jinsi hiyo kama Baba Mungu.
Ina maana kwamba tunakufa katika uhusiano wote uliopita kwamba kuanzia sasa na
kuendelea maisha yetu ni ya kumtegemea Yeye.
Kubatizwa katika Roho Mtakatifu ina maana kwamba unakufa kwa yale yaliyopita.
Uhusiano wako wa zamani unaondolewa. Ninatunzwa katika Yeye, kuishi na kutembea
katika ushirika naye.
Hekima yake ni ya kuchukua nafasi ya ujinga wangu, nguvu yake ni ya kuchukua nafasi
ya udhaifu wangu, uzuri wake ni wa kuchukua nafasi ya kushindwa kwangu.
Kwa maneno mengine nimetambulishwa kikamilifu na kabisa katika mmoja na Yeye
ambaye hawezi kana kwamba ninaishi, bali Yeye ambaye huishi maisha yake katika
mimi.
Kubatizwa katika Jina la Bwana Yesu Kristo ni la kitajiri na kikamilifu zaidi ya hayo-
lina unganisha yote ambayo yapo katika hayo pamoja na nyongeza.
Wakati ninapobatizwa katika Kristo, ninamvaa Kristo sasa ni haki mbele za dunia na
mbele za mbinguni -Kristo. Ubatizo kwa maana hii unalingana na ndoa.
Wakati mwanamke anapo olewa anachukua jina la mume wake na kuingia katika milki
ya mume wake na haki zake za halali nyumbani kwa mume wake.
Wakati mwamini anapobatizwa katika Jina la Yesu anavaa yote ambayo yapo katika
Kristo. Havai tu lile jina bali anachukua haki zote za halali na upendeleo katika Kristo.
Wakati mwanamke anapoolewa katika jina la mume wake ameolewa katika utajiri wake,
heshima na utukufu na kutambuliwa pamoja na yeye katika yote ambayo alikuwa nayo
na hata yale atakayokuwa nayo.
Kwa hiyo wakati tunapobatizwa katika jina la Bwana Yesu, tunabatizwa katika yote
ambayo lile jina unasimama kwalo, utajiri wake wote, heshima yako yote, nguvu zake
zote, utukufu wote uliopita na ujao. Yote ambayo jina linasimama kwayo mbinguni ni
yetu. Kila ushindi ambao alishinda katika kifo chake, mateso, na kuzimu hadi kufufuka
kwake ni yetu.
Yote, Yote, ni Yetu
Hakushinda ushindi wowote katika kazi yake badala yetu ambao haukuwa kwa ajili ya
faida ya wale walioungana na Yeye katika ubatizo.
Yote ambayo jina linasimama kwayo mbele za Baba ni mali ya mwamini.
Tunabatizwa katika haki halali kutumia jina katika upendeleo wa jina hilo, katika wajibu
wote wa mwana uliotunukiwa pamoja na nguvu ya kipekee ya jina lile kuu.
Wakati aliposema “Nimepeawa mamlaka yote mbinguni na duniani” basi enendeni
mkawafanye mataifa kuwa wanafunzi, basi mamlaka yale aliyokuwa nayo ni yetu-
tunasimama kama wawakilishi wake tunaenda katika ulimwengu huu tukiwa na jina
lake.
Tunabatizwa katika haki yake, katika ufufuo wake nguvu na utukufu.
Sasa haki yake ni yetu, neema yake ni yetu, upendo wake ni wetu, nguvu zake ni zetu,
ndiyo yeye mwenyewe ni wetu. Je, sisi ni matajiri kiasi gani?
Sasa kutumia jina hili haihitaji imani yoyote maalum au isiyo kawaida kwa sababu ni
letu. Kama waamini utajiri wote na neema ni mali yetu. Hakuna tendo maalum katika
sehemu ya Mungu. Hakuna maandalizi maalum katika sehemu yetu ambayo ni lazima
wakati baadhi ya matatizo makubwa yanapotokea - lile jina ni letu, tulilopewa kihalali
kutumia dhidi ya majeshi ya adui za Mungu, na tunasimama tukifunikwa katika haki,
upendeleo, na nguvu za mwana wa Mungu.
Hatuhitajiki kutumia imani yeyote ya dhamira - yote ambayo tunatakiwa kufanya ni
kutumia jina.
Uliamriwa na Kristo
1. Mkibatiza Mat. 28:19
2. Aaminiye na kubatizwa Marko 16:16
Ulifanywa na Mitume na watu wengine
1. Na mitume wa kwanza. Mdo 2:38, 41
2. Na Paulo, Mdo 19:1-5
3. Na Petro na Mataifa, Mdo 10:45-48
4. Na Filipo na Towashi, Mdo 8:36-38
5. Na Anania Sauli, Mdo 9: 17-18
Kwa kufuata hali fulani za kiroho
1. Toba, Mdo 2:38
2. Imani katika Neno, Mark 16:15, 16; Mdo 2:41; 16:14,15
3. Imani katika Kristo, Mdo 8:12,35-38; 19:4; 16:31-33
Ilionesha maana fulani za kiroho
1. Sio kama ubatizo wa Yohana, Mdo 19:3-5
2. Ishara ya kutambulisha jina la utatu wa Mungu, Mat. 28:19
3. Ishara ya kutambulisha kwa njia ya Roho jina la nafsi ya Kristo. Mdo 8:16, 19:5, 1Kor.
12:13
4. Ishara ya kumvaa Kristo, Wagalatia 3:27, Warumi 6:3
5. Ishara ya kutambuliwa na Kristo katika kifo, kuzikwa na kufufuka, Warumi 6:3-5
Kwa maelezo zaidi kuhusu ACMTC TANZANIA, au jinsi utakavyoweza
kujihusisha, wasiliana na Meja Frank & Elina Materu: S.L.P. 7579 Dar es
Salaam, Tanzania. Barua pepe: materufrank@yahoo.com
|